Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China laanza kikao chake cha mwaka
2023-03-04 16:25:08| cri

Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China CPPCC limeanza kikao chake cha mwaka leo Jumamosi mchana hapa Beijing.

Rais Xi Jinping na viongozi wengine wa China wamehudhuria mkutano wa ufunguzi wa kikao cha kwanza cha Kamati ya 14 ya Taifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), ambacho ni chombo cha ngazi ya juu zaidi cha mashauriano ya kisiasa cha China.

Wang Yang, mwenyekiti wa Kamati ya 13 ya Taifa ya CPPCC, aliwasilisha ripoti ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya Kamati hiyo ya Taifa ya CPPCC kwenye kikao hicho.