Mkutano wa Bunge la Umma la China wafunguliwa Beijing
2023-03-05 10:39:53| CRI

Mkutano wa kwanza wa awamu ya 14 ya Bunge la Umma la China umefunguliwa Jumapili hapa Beijing, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo rais wa China, Xi Jinping.

Katika mkutano huo, Waziri Mkuu Bw. Li Keqiang ametoa ripoti ya kazi ya serikali, ambapo amesema mwaka 2022 ulikuwa ni mwaka muhimu katika historia ya Chama cha Kikomunisti cha China na taifa. Amesema Mkutano Mkuu wa 20 wa Wajumbe Wote wa Chama cha Kikomunisti cha China ulifanyika kwa mafanikio, na kuweka mipango kuhusu ujenzi wa nchi ya ujamaa wa kisasa kwa pande zote.

Pia amesema, ili kukabiliana na mazingira yenye utatanishi ya kimataifa, na kazi ngumu ya mageuzi, na kuimarisha maendeleo na utulivu nchini, Kamati Kuu ya Chama ikiongozwa na rais Xi Jinping imewaongoza Wachina kukabiliana na changamoto na kutekeleza kikamilifu kazi ya kuzuia janga la COVID-19, kutuliza hali ya uchumi na kuhakikisha maendeleo kwa usalama, kuongeza nguvu ya udhibiti na marekebisho katika hali ya jumla, na uchumi umeendelea vizuri, ubora wa maendeleo umeinuka kwa kasi, na utulivu wa kijamii umedumishwa.