Vipindi maalum vya Mikutano Miwili (1)
2023-03-06 16:31:52| CRI

Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita yaani baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC, katika kipindi cha Mikutano Miwili ya kila mwaka, rais wa China na Katibu Mkuu wa kamati kuu ya CPC Xi Jinping anajadiliana na wajumbe mbalimbali juu ya masuala ya taifa. Na katika mfululizo wa kauli zake muhimu, Xi ametumia mashairi au misemo ya kale na kuhusisha utamaduni bora wa jadi wa China katika nadharia na utendaji wa utawala wa nchi.

1.   “Upepo unapiga majani, nasikia kama watu wanalia” (shairi alilonukuu Xi Jinping alipokutana na wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa kutoka sekta za kilimo, ustawi wa jamii tarehe 6 Machi 2022)

Ustawi wa vijiji haumaanishi kuleta maendeleo ya kiuchumi tu, lakini pia ni lazima kuzingatia mila bora za vijiji, familia na watu. Kazi hii inapaswa kufanywa kama ya kawaida. “Hakuna jambo dogo katika masuala yanayohusu maisha ya watu, na upepo unapiga majani, nasikia kama watu wanalia.”

2.   “Kufanya maamuzi kulingana na hali halisi, kutumia vizuri nguvu bora na kufidia udhaifu” (msemo wa kale alionukuu Xi Jinping alipohudhuria na kutoa hotuba kwenye mjadala ya wajumbe wa Qinghai kwenye Mkutano wa 4 wa Bunge la 13 la Umma la China)

Maendeleo ya hali ya juu sio tu yapo kwenye sekta ya uchumi peke yake, bali pia yapo katika sekta zote za maendeleo ya kiuchumi na kijamii; sio tu yapo kwenye kanda zilizoendelea kiuchumi, lakini pia ni maagizo ambayo lazima yatekelezwe kote nchini; sio maagizo ya muda fulani, lakini yanatakiwa kutekelezwa kwa muda mrefu. Kila eneo linapaswa kuzingatia hali halisi, “kufanya maamuzi kulingana na hali halisi, kutumia vizuri nguvu bora na kufidia udhaifu” na kutafuta njia ya kutafuta maendeleo ya hali ya juu inayolingana na hali halisi ya eneo hilo.