Emir wa Qatar atoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono utekelezaji wa Mpango wa Doha
2023-03-06 20:56:52| cri

Mkutano wa tano wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya nchi zenye maendeleo duni zaidi duniani, umefunguliwa mjini Doha nchini Qatar. Emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani ametoa wito kwenye mkutano huo kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono na nchi zenye maendeleo duni zaidi katika utekelezaji wa Mpango wa Doha (DPoA) ili kuzisaidia kupata maendeleo endelevu.

Nchi zenye maendeleo duni zaidi duniani zinatajwa na Umoja wa Mataifa kuwa ni nchi zilizo chini zaidi kwenye viwango vya maendeleo ya uchumi na jamii na Vigezo vya Maendeleo ya Binadamu (HDI). Hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu, nchi 46 duniani zimeorodheshwa kuwa nchi zenye maendeleo duni na 33 kati yao ni nchi za Afrika.