Rais wa Tanzania atoa ardhi kwa ujenzi wa makao makuu ya EABC
2023-03-06 08:36:30| cri


 

Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) hivi karibuni lilitoa taarifa likisema, rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa hekta tatu za ardhi kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu ya Baraza hilo mjini Arusha. 

Ijumaa iliyopita, rais Samia alikabidhi hati ya ardhi hiyo iliyoko eneo la Matves kwa mkurugenzi mtendaji wa EABC John Kalisa. Taarifa hiyo imesema, hatua hiyo itawezesha EABC kujenga makao makuu yake huko Arusha, ambayo pia ni makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).