Xi ashiriki kwenye majadiliano ya wajumbe wa CPPCC
2023-03-06 17:10:56| CRI

Leo mchana, rais Xi Jinping wa China na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC ameshiriki kwenye majadiliano ya pamoja ya wajumbe wa Chama cha Ujenzi wa Demokrasia cha  China na Shirikisho la viwanda na biashara la China, akisikiliza maoni na mapendekezo ya wajumbe hao wanaohudhuria kwenye mkutano wa kwanza wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la China CPPCC unaoendelea hapa Beijing.