Kwa nini Xi Jinping amesisitiza mara nyingi maendeleo yenye ubora wa juu?
2023-03-06 16:03:44| cri

Mkutano mkuu wa bunge la umma la China ulifunguliwa Machi 5 hapa Beijing. Rais Xi Jinping wa China amehudhuria mjadala wa ujumbe wa mkoa wa Jiangsu waliojadili ripoti ya kazi ya serikali, huku akisisitiza tena kushikilia jukumu la kwanza la kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu.

Katika miaka ya hivi karibuni, rais Xi ametaja mara nyingi matakwa ya maendeleo yenye ubora wa juu katika hotuba zake, huku akitoa maagizo ya kazi husika katika mikutano muhimu kadhaa. Maendeleo yenye ubora wa juu ni madhumuni muhimu katika mipango ya uchumi, yakilenga kuhimiza kuinuka kwa kiwango cha uchumi wa China.

Kipaumbele cha maendeleo yenye ubora wa juu ni kuharakisha kutimiza lengo la kujitegemea kwa teknolojia ya hali ya juu. Kwa mujibu wa rais Xi, hii ni njia ya lazima ya kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu, pia ina umuhimu utakaoifanya China iweze kujijenga kwa pande zote kuwa nchi ya kisasa ya kijamaa.

Katika mazingira ya kimataifa yenye ushindani mkali, Marekani inashirikiana na washirika wake kuzuia maendeleo ya China katika sekta ya teknolojia ya hali ya juu, huku ikiziweka makampuni ya China kwenye orodha ya vikwazo. Hivi sasa kama China ikitaka kutimiza maendeleo yenye ubora wa hali ya juu, kufungua njia mpya na kuleta msukumo mpya kwenye maendeleo yake, kimsingi itategemea uvumbuzi wa teknolojia.