Utimiaji wa mambo ya kisasa kwa njia ya China kutoa fursa kwa dunia nzima
2023-03-06 10:35:23| CRI

Mikutano Miwili Mikubwa ya nchini China, mkutano wa Bunge la Umma la China na mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China imefunguliwa, na jamii ya kimataifa inafuatilia jinsi China itakavyosukuma mbele maendeleo ya mambo ya kisasa kwa njia ya China .

Katika tahariri yake, Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) limesema utimiaji wa mambo ya kisasa kwa njia ya China  utatoa fursa kwa dunia nzima.

Tahariri hiyo imesema ripoti ya kazi za serikali iliyotolewa kwenye mkutano wa Bunge la Umma la China imetangaza lengo la maendeleo ya uchumi la mwaka huu, ambalo limeongeza ushawishi kwa uchumi wa dunia unaokabiliwa na changamoto ya kudidimika.

Tahariri hiyo imesisitiza kuwa, hivi sasa China inakabiliwa na hali ya kutatanisha ya kimataifa, lakini mwelekeo mzuri wa muda mrefu wa uchumi wake haujabadilika, na Wachina wana imani kuwa na mustakabali mzuri kutokana na juhudi zao, na kupata mafanikio ya pamoja na dunia nzima.