Wizara ya Ulinzi ya Zambia imewatunukia wataalam 11 wa timu ya 25 ya kijeshi ya matibabu ya China nchini Zambia "Nishani ya Ushirikiano wa kirafiki wa kimataifa".
Katibu wa kudumu wa Wizara ya Ulinzi wa Taifa ya Zambia Bw. Chipa Kupaku amesema, Zambia inalishukuru kwa dhati jeshi la China kwa kutuma timu ya wataalam wa ngazi ya juu wa matibabu nchini Zambia kwa muda mrefu, na anatarajia kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na China katika nyanja mbalimbali ikiwemo matibabu.
Kwa upande wake, mjumbe wa kijeshi wa Ubalozi wa China nchini Zambia, Bw. Jiang Lei amesema, madaktari wa kijeshi wa China wataendelea kuendeleza moyo wa kutoogopa matatizo, kuwatibu wenyeji kwa moyo wa kujitolea, na kutoa mchango mkubwa zaidi katika kukuza ushirikiano wa kivitendo kati ya majeshi na kuimarisha urafiki kati ya watu ya nchi hizo mbili.