China yalishauri Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuondoa vikwazo dhidi ya Sudan Kusini
2023-03-07 08:34:24| cri

Naibu mjumbe wa China katika Umoja wa Mataifa, Balozi Dai Bing amesema, Baraza la Usalama linapaswa kuondoa mara moja vikwazo dhidi ya Sudan Kusini.

Akizungumza katika kikao maalum cha Baraza hilo kuhusu Sudan Kusini hapo jana, Balozi Dai amesema, ghasia katika maeneo mengi ya Sudan Kusini zimeongezeka, na hali ya usalama na kibinadamu inatia wasiwasi. Amesema China inatoa wito kwa pande zote husika kuacha mara moja mapambano na kutatua tofauti zilizopo kwa njia ya mazungumzo na kuongeza kuwa, vikwazo vilivyowekwa na Baraza hilo vimepunguza uwezo wa serikali ya Sudan Kusini kulinda raia.