Kenya kupanua ufikishaji wa chanjo ya malaria
2023-03-07 22:28:39| cri

Wizara ya Afya ya Kenya imetangaza kuwa itaongeza ufikishaji wa chanjo ya malaria nchini humo, ambao unatarajiwa kuzifikia wilaya 25 kwa jumla na kazi ya utoaji itaanzia tarehe 7 mwezi huu.

Wizara hiyo imeeleza kuwa chanjo itakayotolewa ni aina ya RTS,S, ambayo ni chanjo ya kwanza dhidi ya malaria duniani. Tangu mwaka 2019, Kenya imetoa dozi zaidi ya milioni moja za chanjo ya malaria katika wilaya 8 zilizoko magharibi mwa nchi hiyo, na watoto takriban laki 4 wamepokea chanjo hiyo.