Waziri wa mambo ya nje wa China ajibu maswali kuhusu “sera ya diplomasia ya China na uhusiano na nje”
2023-03-07 15:20:30| cri

Mkutano wa  Bunge la umma la 14 la China umefanya mkutano nawaandishi wa habari , na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang amejibu maswali ya  waandishi wa habari wa ndani na nje kuhusu “sera ya diplomasia ya China na uhusiano na nje”.

Bw. Qin Gang akizungumzia ujenzi wa mambo ya kisasa ya China wenye umaalumu wa China, amesema China yenye watu bilioni 1.4 kuelekea kuwa nchi ya kisasa kwa ujumla kutakuwa ni mwujiza ambao haujawahi kutokea katika historia ya binadamu, na kutakuwa na  umuhimu mkubwa kwa dunia nzima. Ujenzi wa mambo ya kisasa wenye mtindo wa China umetatua masuala mengi yanayoyakabili maendeleo ya jamii ya binadamu, na kuvunja wazo potofu la “kuwa kisasa ni sawa na kuwa kimagharibi”, huku ukivumbua mtindo mpya wa ustaarabu wa binadamu na kutoa wazo muhimu kwa nchi zinazoendelea.

Bw. Qin alipozungumzia uhusiano kati ya China na Russia, amesema baadhi ya nchi zimezoea kufikiria uhusiano huo kwa wazo la vita baridi. Uhusiano kati ya China na Russia umejengwa  kwenye msingi wa kutofungamana na kutolenga upande wa tatu, ambao hautakuwa tishio kwa nchi yoyote duniani, pia hauruhusiwi  kuchokozwa na kusumbuliwa na upande mwingine wowote. Mshikamano kati ya China na Russia umetia nguvu katika kuijenga dunia iwe na ncha nyingi na kuyafanya mahusiano ya kimataifa yawe ya kidemokrasia, na kutoa uhakikisho kwa uwiano na utulivu wa kimkakati duniani.

Akizungumzia suala la Taiwan, Bw. Qin amesema kutatua suala la Taiwan ni jambo la watu wa China, na nchi yoyote haina haki ya kuingilia. Amenukuu Katiba ya Jamhuri ya Watu wa China ikisema Taiwan ni sehemu moja ya ardhi ya China. Kufanikisha  muungano wa taifa ni jukumu la pamoja la watu wote wa China wakiwemo ndugu wa Taiwan.