Ghana imefanya sherehe za kuadhimisha miaka 66 ya uhuru tarehe 6 Juni huko Adaklu. Askari wa vikosi vya Jeshi la majini, nchi kavu na anga la Ghana, na wale wa polisi, kikosi cha zima moto, na wajumbe wa walimu na wanafunzi walishiriki kwenye gwaride. Rais wa Ghana Nana Akufo Addo, maofisa waandamizi wa serikali na jeshi na watu kutoka sekta mbalimbali za jamii walihudhuria sherehe hiyo.