Watu 11 wakiwemo wanajeshi na wasaidizi wao wameuawa Jumamosi katika shambulizi dhidi ya kikosi cha kijeshi kaskazini magharibi mwa Burkina Faso.
Shirika la habari la Burkina Faso (AIB) limeripoti kuwa, magaidi kadhaa wakiwemo viongozi waliuawa Jumapili katika mashambulizi yaliyotokea mashariki na maeneo ya kaskazini na katikati mwa nchi hiyo.
Burkina Faso imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa usalama tangu mwaka 2015, huku watu wengi wakiuawa na maelfu ya wengine kuyakimbia makazi yao.