Rais Xi Jinping atoa salamu kwa wanawake wa China wakati Siku ya Wanawake Duniani ilikaribia
2023-03-07 15:26:59| cri

Rais Xi Jinping jana mchana aliwatembelea wajumbe wa Chama cha Ujenzi wa Demokrasia la China na Shirikisho la viwanda na biashara wanaohudhuria kwenye mkutano wa kwanza wa Baraza la 14  la Mashauriano ya Kisiasa la China CPPCC, pia alishiriki kwenye majadiliano ya pamoja akisikiliza maoni na mapendekezo ya wajumbe hao.

Wakati Siku ya Wanawake Duniani ilipokuwa inakaribia, akiwa kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti China, Rais Xi Jinping ambaye pia ni katibu mkuu wa kamati kuu ya chama ametoa salamu kwa wajumbe, makamishina na wafanyakazi wanawake wanaohudhuria  kwenye “Mikutano Miwili” ya China, wanawake wa China kutoka makabila na sekta mbalimbali, ndugu wanawake wa mikoa ya utawala maalumu ya Hong Kong na Macao na mkoa wa Taiwan, pamoja na Wachina wanawake wanaoishi katika nchi za nje.