Watu 9 wauawa katika shambulizi la kujitoa mhanga Kusini Magharibi mwa Pakistan
2023-03-07 08:44:52| cri


 

Polisi wa Pakistan walisema, watu 9 wameuawa na wengine 10 kujeruhiwa katika shambulizi la kujitoa mhanga lililotokea jana mkoani Balochistan, kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Polisi wamesema, mshambuliaji alipanda pikipiki iliyotegwa mabomu na kugonga lori lililobeba askari 22. Mpaka sasa hakuna kundi lolote au watu binafsi waliokiri kuhusika na shambulizi hilo.