Rais wa China asisitiza maendeleo ya ubora wa juu yenye afya katika sekta binafsi
2023-03-07 08:42:39| CRI

Rais wa China Xi Jinping ametaka mwongozo sahihi kwa ajili ya maendeleo ya ubora wa juu yenye afya ya sekta binafsi.

Rais Xi amesema hayo alipokutana na wajumbe wa kisiasa wa kitaifa kutoka Shirikisho la Ujenzi wa Demokraisa la Taifa la China na Shirikisho la Viwanda na Biashara la China, ambao wanashiriki kwenye kikao cha kwanza cha Baraza la 14 la Mashauri ya Kisiasa la China (CPPCC), ambapo alishiriki kwenye majadiliano yao na kusikiliza maoni na mapendekezo yao.

Rais Xi amesisitiza kuwa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) daima bila kusita inaimarisha na kuendeleza sekta binafsi, na inatia moyo, kuunga mkono na kuongoza maendeleo ya sekta isiyo ya kijamii.

Pia, rais Xi ametoa salamu na kuwatakia wanawake wote wa makabila yote na wa ngazi zote za maisha nchini China heri ya Siku ya Wanawake Duniani, ambayo inaadhimishwa Machi 8 kila mwaka.