Mpango wa Ukanda Mmoja na Njia Moja ni bidhaa ya umma ya hali ya juu
2023-03-08 08:48:27| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang amesema, Mpango wa Ukanda Mmoja na Njia Moja (BRI) ni bidhaa ya umma ya hali ya juu ulioanzishwa na China na kujengwa kwa pamoja na washirika wote, na faida zake zimenufaisha dunia. 

Qin amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari kando ya Mkutano wa kwanza wa Bunge la 14 la Umma la China. Amesema katika muongo mmoja uliopita, BRI imefanya uwekezaji wa karibu dola za kimarekani trilioni moja, kujenga miradi ya ushirikiano zaidi ya elfu tatu, kutoa nafasi za ajira zaidi ya laki 4.2 katika nchi zilizojiunga na mpango huo, na kusaidia kuwaondoa karibu watu milioni 40 kutoka kwenye umaskini. 

Akijibu madai kuwa BRI inaweza kuleta mitego ya madeni, Qin amesema China kamwe haipaswi kushutumiwa kwa kuleta mitego ya madeni, na kwamba taasisi za fedha za kimataifa, na wakopeshaji wa kibiashara zinachangia zaidi ya asilimia 80 ya madeni ya nchi zinazoendelea. 

Amesema mwaka huu China ni mwenyeji wa Mkutano wa tatu wa ushirikiano wa kimataifa wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, na itachukua fursa hiyo kushirikiana na pande zote ili kuleta matokeo mazuri kwa ushirikiano wa Ukanda Mmoja na Njia Moja.