Mshauri wa rais wa Senegal asema nchi za magharibi zinachochea mapambano kati ya Russia na Ukraine
2023-03-08 20:38:09| cri

Mapambano kati ya Russia na Ukraine yanaendelea kwa muda mrefu, lakini nchi za magharibi zinaipatia Ukraine silaha badala ya kuhimiza kufanya mazungumzo ili kusimamisha mapambano hayo. Mshauri wa rais wa Senegal alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) amesema, nchi za magharibi kama Marekani zinachochea mapambano hayo, hali ambayo inaleta wasiwasi mkubwa zaidi.

Mshauri huyo amesema mashirika na makundi yanayohusu mambo ya kijeshi kutoka nchi za magharibi pamoja na makundi husika ya kijamii ya Ulaya na Marekani yanachochea mapambano hayo, lakini dunia inahitaji amani badala ya vita. Kwa sasa nchi hizo za magharibi zinaendelea kutunga mkakati kwa ajili ya vita bila kuona kuwa amani ni sharti la lazima kwenye mfumo wa utatuzi wa migogoro duniani, hali ambayo inaweza kuleta matatizo.