Kikao cha pili cha mkutano wa Bunge la Umma la China chafanyika
2023-03-08 08:44:33| cri

Bunge la Umma la 14 la China (NPC) jana limefanya kikao cha pili cha mkutano wake na kusikiliza ripoti za kazi zilizotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la 13, Mahakama Kuu ya Umma ya China (SPC) na Idara Kuu ya Uendeshaji Mashtaka ya China (SPP), pamoja na maelezo kuhusu mageuzi ya  vyombo vya Baraza la Serikali.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la 13 Bw. Li Zhanshu alitoa ripoti kuhusu kazi za bunge hilo, huku Jaji Mkuu Zhou Qiang akitoa ripoti kuhusu kazi ya SPC, na mwendesha mashtaka mkuu Zhang Jun alitoa ripoti kuhusu kazi ya SPP.

Mjumbe wa taifa Bw. Xiao Jie alitoa maelezo kwa bunge hilo kuhusu mpango wa mageuzi ya taasisi za Baraza la Serikali.