Shirika la “Save the Children”: takriban robo ya watoto wa Umoja wa Ulaya wanakabiliwa na hatari ya umaskini
2023-03-08 21:37:34| cri

Shirika la hisani la kimataifa “Save the Children”, limetoa ripoti ikisema takriban robo ya watoto wa Umoja wa Ulaya wanakabiliana na tishio la umaskini, hali ambayo inamaanisha kuwa watoto takriban milioni 20 walioko katika eneo la Umoja wa Ulaya wanaishi katika hali iliyo karibu na umaskini.

Ripoti hiyo imesema kutokana na ongezeko la gharama za maisha na mabadiliko ya tabianchi, idadi ya watoto wa Umoja wa Ulaya wanaokabiliwa na tishio la umaskini inaongezeka kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni. Msukosuko wa gharama za maisha unaosababishwa na mapambano kati ya Russia na Ukraine na athari nyingine zinazoambatana, vinaleta changamoto kubwa za kimaisha kwa familia zenye mapato ya chini na ya kati katika Umoja wa Ulaya.