Jukumu la Majaji na Mahakimu Wanawake katika kuleta haki
2023-03-17 08:00:32| CRI

Licha ya kuongezeka kwa ushiriki wa wanawake katika masuala ya umma, lakini linapokuja suala la kutoa maamuzi uwakilishi wa wanawake huwa ni mdogo sana. Kwa ujumla, suala la idadi ndogo ya wanawake hasa katika nyadhifa za juu za uongozi wa mahakama limekuwa ni jambo lililozoeleka. Ikumbukwe kuwa uwakilishi wa wanawake katika mahakama ni muhimu katika kuhakikisha kwamba mahakama zinawakilisha raia wao, kushughulikia matatizo yao na kutoa hukumu nzuri. Hivyo uwepo wao tu, basi huongeza uhalali wa mahakama, na kutoa ujumbe wenye nguvu kwamba mahakama hizi ziko wazi na kufikiwa na wale wanaotafuta njia ya kupata haki.

Kuingia kwa majaji wanawake katika nafasi ambazo walikuwa wametengwa kihistoria imekuwa hatua chanya katika mwelekeo wa mahakama kuzingatiwa kuwa ziko wazi zaidi, jumuishi, na kuwakilisha watu ambao maisha yao yanaguswa na mahakama hizo. Siku ya Majaji Wanawake ya Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa Machi 10, ambapo huu ukiwa ni mwaka wa pili, inathibitisha dhamira ya kuandaa na kutekeleza mikakati na mipango ya kitaifa ifaayo na madhubuti ili kuwaendeleza wanawake katika mifumo ya haki ya mahakama na taasisi katika ngazi za uongozi, usimamizi na ngazi nyinginezo. Hivyo leo katika kipindi cha Ukumbi wa Wanawake tutaangazia suala zima la majaji wanawake.