Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mashirika ya kuhudumia wakimbizi ya Ethiopia yamesema takriban watu laki 1 wamekimbia mapigano katika eneo lililojitenga la Somalia la Somaliland hadi kwenye eneo la mbali lililokumbwa na ukame nchini Ethiopia la Doolo, lililoko kusini mashariki mwa nchi hiyo.
Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema linaamini kuwa zaidi ya watu 98,000 wamevuka mpaka tangu Februari 6.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wakimbizi na Waliorejea wa Ethiopia (RRS), amesema eneo hilo ambalo halina miundombinu na lina maendeleo duni ya kijamii, limekumbwa na ukame ambao umedumu kwa miaka minne.
Ofisa wa UNHCR nchini Ethiopia Bw. Mamadou Dian Balde amesema licha ya kuwa bado hawajaweza kuwafikia watu wa huko ambao wamekuwa wakikaa majumbani mwao, na walikuwa wakigawana chakula walichokuwa nacho.