Sudan Kusini yatangaza mlipuko wa kipindupindu
2023-03-09 08:49:53| cri


 

Sudani Kusini imetangaza mlipuko wa kipindupindu baada ya kuthibitisha sampuli mbili kwenye eneo la uhifadhi wa raia (POC) huko Malakal, mji mkuu wa jimbo la Upper Nile.

Waziri wa Afya nchini humo Yolanda Awel Deng amesema, tarehe 22 mwezi Februari, Wizara yake ilipokea tahadhari ya mlipuko wa kipindupindu huko Malakal, na kuunda timu ya majibu ya haraka iliyoshirikisha pande zote ili kufanya uchunguzi wa awali na uthibitisho kuhusu ugonjwa huo, na kuunga mkono majibu ya awali.

Amesema, tangu Februari 22, maofisa wa afya wamerekodi kesi 179 za kipindupindu na kifo kimoja katika mji wa Malakal, na kuongeza kuwa, asilimia 59 ya kesi hizo ni wanaume na asilimia 41 ni wanawake, huku watoto walio na umri wa chini ya miaka minne wakiathiriwa zaidi na ugonjwa huo.