Xi asisitiza kuimarisha mikakati ya kitaifa na uwezo wa kimkakati
2023-03-09 14:59:59| cri

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kufungua uwanja mpya wa kuimarisha mikakati jumuishi ya taifa na uwezo wa kimkakati.

Rais Xi amesema hayo alipohudhuria mkutano mkuu wa ujumbe wa Jeshi la Ukombozi la Umma (PLA) na Jeshi la Polisi la Umma, wakati wa mkutano wa kwanza wa bunge la 14 la umma la China.

Rais Xi amesema, kuunganisha na kuimarisha mikakati jumuishi ya taifa na uwezo wa kimkakati kuna umuhimu mkubwa katika kujenga nchi ya kisasa ya kijamaa katika nyanja zote na kuhimiza ustawishwaji mkubwa wa taifa la China kwa pande zote, pamoja na kutimiza malengo ya karne ya jeshi la PLA katika mwaka 2027 na kuinua haraka kiwango cha vikosi vya jeshi hadi kufikia viwango vya dunia.

Akisisitiza lengo la kuinua kwa kiasi kikubwa zaidi uwezo wa kimkakati wa taifa wa China, rais Xi ametoa mwito wa kufanywa juhudi za kuratibu mpangilio wa kimkakati, rasilimali na nguvu katika maeneo mbalimbali, ili kuongeza uwezo wa jumla wa nchi wa kukabiliana na changamoto za kimkakati, kulinda maslahi ya kimkakati na kutimiza malengo ya kimkakati.