Kamishna wa Umoja wa Afrika atoa wito wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika sekta ya teknolojia
2023-03-09 08:51:19| CRI

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat ametoa wito wa kuongeza ushiriki wa wanawake na wasichana katika sekta ya teknolojia.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani hapo jana, Faki amesema kaulimbiu ya Siku hiyo, “Ubunifu wa Teknolojia: Kwa Usawa wa Jinsia-Miaka 20 ya Mkataba wa Maputo”, inaendana na vipaumbele kadhaa vya Umoja huo.

Amesisitiza kuwa, ajenda ya maendeleo ya Umoja huo haitaweza kufanikiwa kama mchango wa wanawake katika maeneo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Sanaa na Hesabu (STEAM) hautapewa kipaumbele.