Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania amesema nchi yake itafanya kila juhudi kuhakikisha eneo la Afrika Mashariki linakuwa na amani na usalama.
Rais Samia amesema hayo hivi karibuni alipokutana na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Joseph Ntakirutimana, na kusisitiza kuwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi yanakwenda sambamba na amani na usalama. Amesema Tanzania inafanya kazi kwa bidii kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa watu wa Afrika Mashariki na kuhakikisha kuwa kuna amani na usalama katika kanda nzima.
Bw. Ntakirutima aliyechaguliwa hivi karibuni kuwa spika wa Bunge alimtembelea Rais Samia mjini Arusha. Rais Samia amemwahidi kumuunga mkono katika kuhakikisha kuwa Bunge la 5 linatimiza wajibu wake wa kuendeleza ajenda ya mafungamano ya Afrika Mashariki.