Ofisa wa Botswana asifu Pendekezo la Maendeleo ya Dunia lililotolewa na China
2023-03-10 08:29:45| cri


 

Meneja msaidizi wa Idara ya Rasilimali Watu katika Wizara ya Elimu ya Juu, Utafiti, Sayansi na Teknolojia nchini Botswana, Keneilwe Sharon Tlhako amesema, pendekezo lililotolewa kwenye Mkutano wa Bunge la Umma la China la “kutekeleza Pendekezo la Maendeleo ya Dunia” lina umuhimu mkubwa katika kuhimiza lengo la kuondokana na wa umaskini.

Keneilwe amesema, China ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, uzoefu wake katika kupunguza umaskini ni mfano wa kuigwa na sehemu nyingine katika lengo hilo.