Waziri wa Ujenzi na Makazi nchini Nigeria Bw. Umar El-Yakub, amesema, kukuza ustawi wa pamoja kutatoa msukumo mkubwa kwa maendeleo ya China ya siku za usoni.
Bw. Yakub amesifu pendekezo la China la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", akisema tangu pendekezo hilo lilipotolewa miaka kumi iliyopita, limeboresha miundombinu na kukuza biashara na uwekezaji katika nchi nyingi.
Bw. Yakub pia amesifu maendeleo ya kisasa ya umaalum wa Kichina, na kusema anaamini kuwa, kutafuta njia ya kisasa ya maendeleo inayofaa kwa nchi husika ni swali ambalo kila nchi inapaswa kufikiria, na anatumai kuwa mchakato wa kisasa wa China unaweza kuleta msukumo zaidi kwa dunia.