Watu sita wauawa katika shambulio la risasi nchini Ujerumani
2023-03-10 08:34:26| CRI

Shirika la habari la Ujerumani RTL limesema, watu sita wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, baadhi yao vibaya, katika shambulio la risasi lililotokea katika kanisa moja Alhamisi mjini Hamburg nchini humo. 

Shirika hilo limesema wahusika wa tukio hilo bado hawajakamawa.

Polisi wa huko wamesema operesheni kubwa inaendelea katika eneo hilo, na kwamba hadi sasa hakuna taarifa za kuaminika zinazoonesha sababu ya shambulio hilo.