Zaidi ya mashirika 70 ya kibinadamu yametoa wito kwa wafadhili kutoa msaada wa fedha ili kukabiliana na mgogoro wa njaa nchini Somalia.
Mashirika hayo, ikiwemo Save the Children na Oxfam, yamesema katika barua ya wazi kwa wafadhili kuwa, hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa kabla hali haijakuwa mbaya zaidi.
Ripoti hiyo imesema, baa la njaa linaweza kutokea katika eneo la Baidoa, Mogadishu, na maeneo ya vijijini katika wilaya ya Burhakaba kati ya mwezi April na Juni kama hatua hazitachukuliwa.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ukame umesababisha watu milioni 1.4 kukimbia makazi yao, na karibu mifugo milioni 3.5 kufariki.