Waziri mkuu asema makampuni binafsi ya China yatafurahia mazingira bora na nafasi kubwa kwa ajili ya maendeleo
2023-03-13 15:40:21| cri

Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang amesema sekta binafsi za kibiashara nchini China zitafurahia mazingira bora na nafasi kubwa kwa ajili ya maendeleo.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari leo hapa Beijing, Bw. Li amesema serikali itaongeza juhudi za kukuza mazingira ya kibiashara ambayo kiini chake ni soko, yana msingi wa kisjeria na ya kimataifa, kutendea kwa usawa makampuni ya aina zote za umiliki, na kulinda haki miliki za makampuni na haki na maslahi ya wajasiriamali kwa mujibu wa sheria. Ameongeza kuwa serikali itatoa jukwaa sawa kwa kila aina ya mashirika ya biashara na kusaidia zaidi biashara binafsi kukua na kustawi.

Li amesisitiza kuwa, dhamira ya China katika kukuza maendeleo ya sekta binafsi haina mashaka na ni thabiti.