Rais wa China kuhudhuria mazungumzo ya CPC na vyama vingine duniani
2023-03-13 15:36:52| cri

Msemaji wa Idara ya Mawasiliano na Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Hu Zhaoming ametangaza kuwa, mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya CPC na vyama vya kisiasa vya nchi za nje yatafanyika tarehe 15 kwa njia ya mtandao, ambapo rais Xi Jinping wa China atahudhuria na kutoa hotuba kwenye ufunguzi wa mazungumzo hayo.

Kauli mbiu ya mazungumzo hayo ni “Njia ya kutimiza mambo ya kisasa, majukumu ya vyama vya kisiasa”, na viongozi wa vyama vya kisiasa vya nchi mbalimbali watahudhuria mazungumzo hayo.