Wataalamu na watu mashuhuri 200 duniani watoa wito kuepusha kutokea usambazaji wa chanjo usio na usawa
2023-03-13 09:16:25| CRI

Wataalamu, wasomi na watu mashuhuri takriban 200 kutoka nchi mbalimbali duniani tarehe 11 mwezi huu wametoa barua ya pamoja wakitoa wito kwa nchi mbalimbali kuimarisha ushirikiano katika kuepusha hali ya kukosekana kwa usawa kwenye usambazaji wa chanjo duniani.

Takwimu zilizonukuliwa kutoka jarida la Nature Medicine kwenye barua hiyo, zinaonyesha kuwa kukosekana kwa usawa kwenye usambazaji wa chanjo ya virusi vya COVID-19 mwaka 2021, kulisababisha kifo kimoja katika kila sekunde 24, ambacho kingeweza kuepukika.

Barua hiyo imesema uvumbuzi wa kimatibabu uliofadhiliwa na umma unatakiwa kuchukuliwa kuwa bidhaa ya umma duniani, na kutumika kuboresha afya ya umma na wala sio kukuza faida ya kifedha.    Nchi mbalimbali zinatakiwa kujuta makosa yaliyofanywa katika janga la Covid-19 na kuchukua hatua halisi ili yasitokee tena katika siku za baadaye.