Rais Xi asisitiza kushikilia kwa hatua madhubuti ufunguaji mlango wenye kiwango cha juu
2023-03-13 15:45:09| CRI

Mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China umefungwa leo tarehe 13 hapa mjini Beijing.

Akihutubia ufungaji wa mkutano huo Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuwa, maendeleo ya China yananufaisha dunia, na maendeleo yake hayawezi kupatikana bila ya ushiriki wa dunia. Amesisitiza kuwa ni lazima kuhimiza ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, ili China ijiendeleze kwa kutumia vizuri masoko na rasilimali za dunia, huku ikihimiza maendeleo ya pamoja ya dunia.

Pia ameongeza kuwa China itashikilia bendera ya amani, maendeleo, ushirikiano na kunufaishana, kutekeleza utaratibu halisi wa pande nyingi, na thamani ya pamoja ya binadamu wote, kushiriki kikamilifu kwenye mageuzi na ujenzi wa mfumo wa usimamizi wa dunia, kusukuma mbele ujenzi wa uchumi wa dunia ulio wazi, na utekelezaji wa mapendekezo ya maendeleo na usalama wa dunia.