Rais wa China asisitiza kuhimiza kwa pande zote ujenzi wa mambo ya kisasa ya ulinzi wa taifa na jeshi la kisasa
2023-03-13 15:47:15| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesema ni lazima kuhimiza kwa pande zote ujenzi wa mambo ya kisasa ya ulinzi wa taifa na jeshi la kisasa, na kulijenga jeshi liwe ukuta mkuu wa chuma unaolinda kwa ufanisi mamlaka, usalama na maendeleo ya taifa.

Akihutubia kwenye ufungaji wa Mkutano wa kwanza wa Bunge la 14 la Umma la China uliofanyika leo tarehe 13 mjini Beijing, rais Xi amesisitiza kuwa usalama ni msingi wa maendeleo, na utulivu ni sharti la ustawi. Amesema ni lazima kutekeleza wazo la usalama wa taifa wa jumla, kukamilisha utaratibu wa usalama wa taifa, na kuongeza uwezo wa kulinda usalama wa taifa, na kuinua kiwango cha usimamizi wa usalama wa umma, kukamilisha mfumo wa usimamizi wa jamii, ili kulinda mfumo mpya wa maendeleo kwa kutegemea mfumo mpya wa usalama.