Waziri mkuu asema China na Marekani zinaweza na zinapaswa kushirikiana
2023-03-13 15:42:08| cri

Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang amesema China na Marekani zinaweza na zinapaswa kushirikiana, na kuna mengi ambayo nchi hizo mbili zinaweza kufikia kwa kufanya kazi pamoja.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika baada ya kumalizika kwa mkutano wa kwanza wa Bunge la 14 la Umma la China, Li amebainisha kuwa, kuna baadhi ya watu nchini Marekani ambao wamekuwa wakipiga kauli za “kutengana” na China katika miaka ya hivi karibuni, lakini si watu wengi wanaweza kufaidika na kitendo hicho.

Li amesema China na Marekani zimefungamana kwa karibu kiuchumi, na zote zimefaidika na maendeleo ya upande mwingine.

Amesisitiza kuwa, kipaumbele cha sasa ni kutekeleza kwa vitendo makubaliano yaliyofikiwa na rais Xi Jinping wa China na Joe Biden wa Marekani walipokutana mwezi Novemba mwaka jana.