Bunge la Umma la China laidhinisha baraza jipya la serikali
2023-03-13 08:44:20| CRI

Bunge la Umma la China limeidhinisha baraza jipya la serikali kwenye mkutano wake wa mwaka uliomalizika leo Machi 13.

Baada ya kutetuliwa na waziri mkuu Li Qiang, orodha ya majina ya manaibu waziri mkuu, wajumbe wa Baraza la Serikali, mawaziri, gavana wa benki kuu, mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na katibu mkuu wa Baraza la Serikali, ilipitishwa na wabunge kwenye mkutano wa tano wa kikao cha kwanza cha Bunge la 14 la Umma la China. Rais Xi Jinping amesaini amri ya rais ya kuwateua maofisa hao.

Habari nyingine zinasema nyaraka kadhaa muhimu, zikiwemo rasimu ya ripoti ya kazi ya serikali, rasimu ya azimio kuhusu utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika mwaka 2022 na mpango wa mwaka 2023, rasimu ya azimio kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2022 na bajeti ya mwaka 2023, zimepigiwa kura kwenye mkutano wa leo wa kikao cha kwanza cha Bunge la 14 la Umma la China.