Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita yaani baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC, katika kipindi cha Mikutano Miwili ya kila mwaka, rais wa China na Katibu Mkuu wa kamati kuu ya CPC Xi Jinping anajadiliana na wajumbe mbalimbali juu ya masuala ya taifa. Na katika mfululizo wa kauli zake muhimu, Xi ametumia mashairi au misemo ya kale na kuhusisha utamaduni bora wa jadi wa China katika nadharia na utendaji wa utawala wa nchi.
3. “Watu wenye maslahi sawa na dunia nzima, wanaungwa mkono, lakini wale wanaohodhi maslahi yote ya dunia, wanarubuniwa.” (msemo wa kale wa kichina alionukuu Xi Jinping alipohudhuria na kutoa hotuba kwenye mjadala wa wajumbe wa Bunge la 13 la Umma la China Mei 22, 2020)
Wahenga walisema: “Wale wenye maslahi sawa na dunia nzima, wanaungwa mkono, lakini wale wanaohodhi maslahi yote ya dunia, wanarubuniwa.” Katiba ya Chama cha Kikomunisti cha China inaeleza wazi kuwa Chama hakina maslahi yake binafsi, na kinatanguliza maslahi ya umma wakati wote.
4. “Ndege hawezi kuruka angani kwa ubawa mmoja tu; na farasi hawezi kukimbia kwa kasi kwa mguu mmoja tu.”(msemo wa kale wa kichina alionukuu Xi Jinping alipowatembelea wajumbe wa sekta ya utamaduni na sayansi walioshiriki kwenye mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Machi, 4, 2019.)
“Umma sio dhana dhahania, bali ni mtu mmoja mmoja. Ili kushinda changamoto mbalimbali njiani, na kutimiza malengo yaliyowekwa, ni lazima kutegemea umma kwa karibu.” “Ndege hawezi kuruka angani kwa ubawa mmoja tu; na farasi hawezi kukimbia kwa kasi kwa mguu mmoja tu.” China ikitaka kuruka juu zaidi na kukimbia kasi zaidi, ni lazima kukusanya na kuhamasisha nguvu kubwa za watu bilioni 1.4.