Waziri mkuu wa China asema ana imani kubwa na ukuaji wa uchumi wa China
2023-03-13 13:26:20| CRI

Waziri mkuu wa China Bw. Li Qiang amesema ana imani kubwa na mustakbali wa uchumi wa China, na kwamba utashinda changamoto zitakazojitokeza na kuwa wa kutumainiwa.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano wa kwanza wa Bunge la 14 la Umma la China kufungwa hii leo hapa Beijing, waziri mkuu Li amesema, kuimarisha ukuaji wa uchumi ni kazi yenye changamoto si kwa China pekee bali kwa nchi zote duniani mwaka huu kutokana na hali tete ya dunia kwa sasa. Amesema China imeweka lengo la ukuaji wa uchumi kuwa asilimia 5 kwa mwaka huu kutokana na sababu mbalimbali, na utimiaji wake utahitaji juhudi kubwa.

Ameeleza kuwa China itatumia vyema sera kabambe ikiwa ni pamoja na sera kuu, kuongeza mahitaji, kuendeleza mageuzi na uvumbuzi, na kuzuia na kupunguza hatari zinazoweza kutokea, wakati huohuo, nchi hiyo itaongeza, kurekebisha na kuboresha sera katika mchakato wa utekelezaji.