Tanzania imezindua kituo cha watalii wa kimataifa katika mbuga ya wanyama ya Serengeti, kikilenga kuhimiza vivutio vya utalii vya nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na wizara ya maliasili na utalii imesema, kituo hicho kitatumika kuwapatia watalii habari kuhusu vivutio vya utalii, ramani na vitu vingine vinavyohusiana na utalii.
Waziri wa maliasili na utalii Bw. Mohamed Mchengerwa kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo hicho amesema habari kuhusu mbuga 22 za taifa na hifadhi 29 za wanyamapori za nchi hiyo zitapatikana katika kituo hicho, huku akihimiza wadau wa sekta ya utalii kuiunga mkono serikali katika juhudi zake za kuifanya Tanzania kuwa kituo cha watalii cha kimataifa.