Upigaji kura kwenye uchaguzi wa baraza la Seneti nchini Cameroon wafanyika
2023-03-13 08:45:11| CRI

Upigaji kura kwenye uchaguzi wa baraza la seneti la Cameroon ulifanyika jana kwenye majimbo 10 ya nchi hiyo, huku upigaji kura kwenye vituo 198 vya kupigia kura ukiendelea katika hali ya utulivu.

Tume ya uchaguzi ya Cameroon imesema mameya na madiwani wanachagua maseneta 70 kutoka vyama kumi vinavyoshiriki kwenye uchaguzi huo, na kwamba maandalizi yote muhimu ya vifaa na usalama yalikuwa tayari ili kuhakikisha uchaguzi una kuwa huru na wa haki.

Baraza la Seneti la Cameroon lina viti 100, uchaguzi unafanyika kuchagua maseneta 70, na wengine 30 wanateuliwa na Rais wa nchi hiyo. Uchaguzi wa kwanza wa baraza la seneti katika nchi hiyo ulifanyika mwaka 2013.