Kimbunga cha Freddy chasababisha vifo vya watu 99 nchini Malawi, wakati kazi ya uokoaji inaendelea
2023-03-14 08:58:46| CRI

Mamlaka nchini Malawi zimesema hadi kufikia jana idadi ya watu waliokufa kutokana na kimbunga cha Freddy nchini humo imeongezeka na kufikia 99, na vifo 85 kati ya hivyo vimetokea mjini Blantyre, na maelfu ya watu wakiwa wamepoteza maisha yao.

Kamishna wa idara Usimamizi wa maafa Bw. Charles Kalema amesema watu 134 wamejeruhiwa vibaya, wengine wamejeruhiwa kiasi na kumekuwa na uharibifu mkubwa wa mali katika wilaya 10 ambazo zimeathiriwa zaidi na kimbunga hicho.

Vifo vimetokana na watu kubomokewa na nyumba zao, mafuriko na maporomoko ya udongo. Kimbunga hicho pia kimeharibu miundo mbinu ya kuzalisha umeme, na karibu nchi nzima haina umeme tangu jumatatu.

Habari pia zinasema Msumbiji inajiandaa kukabiliana na madhara ya kimbunga hicho kilichoikumba sehemu ya katikati ya nchi hiyo.