China yasaidia Mashariki ya Kati kutimiza amani, utulivu na usalama
2023-03-14 10:57:17| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran Bw. Nasser Kan'ani, amesema China imeonesha umuhimu mkubwa katika kufanikisha kurudisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Iran na Saudi Arabia, na kusaidia kutimiza amani, utulivu na usalama kwenye eneo la Mashariki ya Kati.

Bw. Kan’ani siku hiyo alisema China ilipokea wajumbe wa Iran na Saudi Arabia kwa nia dhati na kuzisaidia nchi hizo mbili kuwasiliana, na kutoa jukwaa la kufanya mazungumzo na kukubaliana kurudisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, jambo ambalo Iran inashukuru.

Pia amesema kupanua ushirikiano kati ya Iran na Saudi Arabia kunalingana na maslahi ya nchi hizo mbili na pia kutaleta manufaa katika kuhimiza ushirikiano wa kikanda na kimataifa.