Kikao cha mwaka cha Bunge la Umma la China chafungwa Beijing
2023-03-14 08:39:09| CRI

Bunge la 14 la Umma la China limefunga kikao chake cha kwanza cha mwaka jana Jumatatu hapa Beijing.

Akihutubia mkutano wa kufunga kikao hicho, Rais Xi Jinping amesema imani ya umma ni msukumo mkubwa zaidi unaomhimiza kusonga mbele na pia ni wajibu mkubwa anaoubeba.

Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, amesema atatekeleza kwa moyo wote majukumu aliyopewa na Katiba, mahitaji ya taifa yakiwa lengo lake na maslahi ya umma yakiwa kipimo chake.

Rais Xi ameahidi kutekeleza wajibu wake kwa makini, na kufanya kila analoweza kufikia matarajio ya wabunge wote na wananchi wa makabila yote.