Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris atarajiwa kufanya ziara Tanzania, Zambia na Ghana
2023-03-14 22:31:22| cri

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris atatembelea Tanzania, Zambia na Ghana baadaye mwezi huu katika ziara yake ya kwanza barani humo.

Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara za maafisa waandamizi wa serikali ya Marekani ili kuimarisha uhusiano na Afrika huku kukiwa na mchuano mkali wa siasa za kijiografia na mataifa mengine yenye nguvu duniani, yakiwemo China na Urusi.

Ikitoa taarifa ofisi yake ilisema ziara hii itaimarisha ushirikiano wa Marekani kote barani Afrika na kuendeleza juhudi zao za pamoja kuhusu usalama na ustawi wa kiuchumi. Bi Harris atawasili Ghana Machi 26, kisha Tanzania Machi 29 na Zambia Machi 31 hadi Aprili 3. Anatarajiwa kukutana na rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, Samia Hassan wa Tanzania na Hakainde Hichilema wa Zambia na kujadili masuala ya demokrasia, ukuaji wa uchumi, usalama wa chakula na athari za mgogoro wa Ukraine.