Infantino asiye na mpinzani kuwania muhula wa tatu kama rais wa Fifa
2023-03-15 22:55:29| cri

Gianni Infantino anatazamiwa kuwania kwa muhula wa tatu wa miaka minne kama rais wa FIFA wakati Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) litakapofanya mkutano wake wa kila mwaka katika mji mkuu wa Rwanda Kigali siku ya Alhamisi.

Wajumbe kutoka mashirikisho wanachama 211 watakuwa na maamuzi mawili tu katika Mkutano wa 73 wa FIFA, aidha kumchagua tena kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 52 kwa sifa au kukataa kiishara.

Akichaguliwa bila kutarajiwa mwezi Februari 2016 kufuatia kashfa iliyomwangusha Sepp Blatter, Infantino tayari alisimama bila kupingwa kuchaguliwa tena mwaka 2019 na sasa yuko tayari kusalia kusimamia soka ya dunia hadi mwaka 2027.

Wakati sheria za shirikisho hilo lenye makao yake makuu mjini Zurich kwa sasa zikiweka kikomo kwa rais kuwa na hadi mihula mitatu ya miaka minne, Infantino tayari ameandaa mazingira ya kusalia hadi 2031, akitangaza mwezi Disemba kwamba miaka yake mitatu ya kwanza madarakani haikuhesabiwa kama muhula kamili.