Mjumbe wa China: Chuki dhidi ya China itasababisha mgogoro na makabiliano
2023-03-15 08:55:24| CRI

Naibu mwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa Balozi Geng Shuang ameonya kuwa chuki za wanasiasa dhidi ya China zitasababisha mgogoro na makabiliano.

Akiongea kwenye mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu chuki dhidi ya Russia na uhusiano wake na mgogoro wa Ukraine, Balozi Geng Shuang amesema, wanasiasa katika baadhi ya nchi wana mawazo potofu na yenye upendeleo wa kupita kiasi dhidi ya China, wakieneza hofu na kuchochea taharuki. Amesema chuki dhidi ya China (Sinophobia) ni matokeo ya uelewa mbaya kuhusu China, uamuzi mbaya wa kimkakati na mchezo wa kisiasa.
Balozi Geng amesema kama sera ya nchi fulani kuhusu China ikitawaliwa na chuki dhidi ya China, itasababisha kukua kwa mtazamo hasi wa kutoshirikiana unaolenga kunufaisha upande mmoja tu na kudhuru upande mwingine (Zero-Sum Game), na hivyo kuleta mgogoro na makabiliano.