Jumuiya ya makampuni ya China ya Botswana imekabidhi mradi ya kusafisha mtaro wa Segoditshane kwa baraza la mji wa Gaborone, baada ya kazi hiyo iliyoanza Februari 28 kusaidia kukabiliana na mafuriko kukamilika.
Meya wa mji wa Gaborone Bw. Austin Abraham amesema kwenye hafla ya kupokea mradi huo ambayo umetekelezwa kama sehemu ya wajibu wa makampuni kwa jamii, kuwa ni kazi nzuri iliyofanywa na makampuni ya China. Meya huyo amesema kuondoa matope na taka kwenye mtaro wa Segoditshane kutafanya maji yaweze kupita bila kizuizi kwa muda wa miaka miwili ijayo.