vWanakampeni wa Afrika watoa mwito kwa ufugaji bora wa kuku kukabiliana na changamoto za tabia nchi
2023-03-15 09:07:14| CRI

Wanakampeni wamezitaka nchi za Afrika kusini mwa Sahara kufuata mifumo ya ufugaji wa kuku isiyosababisha utoaji wa hewa ya ukaa na kutegemea kemikali za viwandani, ili kuepuka msukosuko wa tabia nchi na kuenea kwa wadudu.

Mkurugenzi wa Afrika wa Shirika la ulinzi wa wanyama (WAP) Bw. Tennyson Williams amesema kufanya ufugaji wa kuku kuwa wa kijani kutahimiza manufaa ya kiikolojia na kiafya kwa bara zima.

Amesema msukosuko wa tabia nchi ni suala halisi barani Afrika, na sekta ya ufugaji wa kuku inatakiwa kuchukua hatua madhubuti ikiwa ni sehemu ya majawabu kwa kulinda vigezo vinavyolinda mazingira ya asili na afya ya binadamu.